1. Leibniz-Zentrum Moderner Orient
  2. Events
  3. Swahili Translations of Foreign Literature: A Case Study of Carlo Collodi's Book Pinocchio (Italy)
Events
Lecture series

Swahili Translations of Foreign Literature: A Case Study of Carlo Collodi's Book Pinocchio (Italy)

Katika wasilisho hili, Flavia Aiello atajadili tafsiri ya fasihi ya kigeni kwa Kiswahili kwa kuzingatia mfano wa tafsiri za Kiswahili za kitabu cha Le avventure di Pinocchio kilichoandikwa na Carlo Collodi na kutolewa Firenze mwaka 1883. Kitabu hiki cha watoto, ambacho kimekuwa maarufu duniani kote na kimetafsiriwa kwa lugha nyingi, kilitafsiriwa kwa Kiswahili mara mbili. Flavia Aiello atalinganisha tafsiri hizi mbili kwa kuzingatia vipengele mbalimbali vya tafsiri kama vile jinsi ya kutafsiri msamiati wa kitamaduni, majina ya wahusika na mahali pamoja na mazingira tofauti ambapo kitabu cha Le avventure di Pinocchio kilitafsiriwa kwa Kiswahili.

Flavia Aiello ni Profesa Mshiriki katika Chuo Kikuu cha Napoli “L’Orientale” ambapo anafundisha lugha na fasihi ya Kiswahili. Eneo kuu la utafiti wake ni fasihi ya Kiswahili ya kisasa (pamoja na vitabu vya watoto) na tafsiri ya kifasihi ya Kiswahili. Amefasiri kazi kadhaa za fasihi ya Kiswahili kwa Kiingereza na hasa kwa Kiitaliano, ikiwemo baadhi ya mashairi kutoka diwani ya Sauti ya Dhiki
ya Abdilatif Abdalla.

Kikao kitafanyika siku ya Jumatatu, tarehe 08 Juli 2024, saa kumi za Ulaya ya Kati (saa kumi na moja za Afrika Mashariki) kupitia njia ya Zoom: https://us02web.zoom.us/j/86897283488?pwd=vNsYUdiKtViP3EPSeyQImV5DzCNLtl.1


KARIBUNI NYOTE!
Tafadhalini wajulisheni wapenzi wote wa Kiswahili na marafiki wengine!
Wasalaam,
Kai Kresse, Lutz Diegner na Maxwell Omondi Ondieki

Kama kuna maswali yoyote kuhusu baraza hili tafadhalini mwandikieni mwenzetu:  MaxwellOmondi.Ondieki(at)zmo.de

This event is part of the lecture series:
Presentation and Discussion Sessions in Swahili 2024
Baraza la Kiswahili la Berlin

Details